October 5, 2021


 IMEELEZWA kuwa mabosi wa Klabu ya Manchester United hawana mpango wa kumfukuza Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solkajaer licha ya kuwa na mwendo mbovu hivi karibuni.

Tayari ndani ya msimu wa 2021/22 amenyooshwa kwenye mechi tatuna amelazimisha sare mbili huku akipata ushindi katika mechi tano ni katika michuano tofauti.

Jina lake limekuwa likitajwa kuwa ni moja ya majina yatakayochimbishwa mapema kutokana na mabosi wa timu hiyo kuwekeza nguvu kubwa kwenye usajili wa nyota wakubwa ikiwa ni pamoja na Cristiano Ronaldo ili aweze kuwapa matokeo ila mambo yamekuwa ni magumu.

Ripoti zinaeleza kuwa licha ya matokeo kuwa mabaya na mwendo mbovu wa timu hiyo iliyo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England pamoja na pointi zake 14 huku vinara wakiwa ni Chelsea wenye pointi 16 bado ripoti zinaeleza kuwa mabosi hawana mpango wa kumfuta kazi kwa kuwa wanaona anafanya vizuri.

Anayetajwa kupewa mikoba ya Solkajaer ni Antonio Conte ambaye kwa sasa yupo huru kwa kuwa hawafundishi tena Inter Milan ambao aliwapa ubingwa walioukosa kwa muda mrefu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic