KICHAPO walichokipaga PSG kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Ligue 1 uliochezwa Oktoba 3 kiliwafanya mastaa wa timu hiyo kuvamiwa na mashabiki wa timu pinzani.
Ikumbukwe kwamba wakati ubao wa Uwanja wa De la Route de Lorient ukisoma Rennes 2-0 PSG mastaa wake wote wakubwa na ghali walikuwa uwanjani.
Mabao ya vijana wa Rennes yalifungwa na Gaetan Laborde dakika ya 45 na Flavien Tait dakika ya 46 jambo lililowafanya PSG kuyeyusha pointi tatu mazima.
Pia rekodi zinaonyesha kuwa PSG ya Lionel Messi na Neymar Jr pamoja na Mbappe ilipiga jumla ya mashuti 13 na hakuna hata moja lililolenga lango huku Rennes wakipiga mashuti 12 na manne yalilenga lango.
Inaelezwa kuwa baada ya mchezo kuisha mashabiki wa Rennes waliwavamia mastaa wa PSG jambo lililowafanya kushindwa kuondoka uwanjani kwa wakati.
Katika msimamo PSG ipo nafasi ya kwanza na ina pointi 24 ikiwa imepoteza mchezo mmoja huku Rennes ikiwa nafasi ya 11 na ina pointi 12 zote zimecheza mechi 9.
Big up to rennes fight together as a team work
ReplyDelete