October 1, 2021


 MSHAMBULIAJI wa Yanga Mkongomani, Heritier Makambo amesikitika kukosa kuwafunga wapinzani wao Simba lakini ameahidi kubeba kiatu cha ufungaji bora katika msimu huu.
 


Staa huyo wa Yanga aliyeingia katika kipindi cha pili akichukua nafasi ya Fiston Mayele, alikosa bao la wazi ndani ya 18 katika dakika ya 90 ukiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii ambao uliisha kwa Yanga kushinda bao 1-0 dhidi ya Simba.


 Akizungumza na Championi Jumatano, Makambo alisema kuwa anaamini uwezo wake wa kufunga mabao, hivyo Wanayanga wasubirie furaha.

Makambo alisema kuwa kitu cha kwanza alichokipanga katika msimu huu ni kuipa ubingwa Yanga wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA baada ya kuyakosa mataji hayo kwa miaka minne na kwenye mafanikio yake binafsi anautaka ufungaji bora.

Pia kwenye mchezo wake wa kwanza wa ligi mbele ya Kagera Sugar alishindwa kufunga na alianzia pia benchi.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilisepa na pointi tatu baada ya kushinda bao 1-0.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic