October 5, 2021


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amefichua kwamba, viwango vinavyooneshwa na mastaa wake wapya, Khalid Aucho na Yannick Bangala, alitarajia kuviona kwani aliamini uwezo wao kabla ya kuwasajili.


Nabi alisema kwamba, baada ya kuwafuatilia kwa kipindi kirefu wachezaji hao, ndipo akapendekeza wasajiliwe, hivyo anaamini watafanya makubwa zaidi ndani ya timu hiyo.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Nabi alisema: “Tumekuwa na mwanzo mzuri wa msimu huu, tayari tumeshinda Ngao ya Jamii, lakini pia tumepata matokeo mazuri katika mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar na ule wa Geita Gold.


 “Kila mtu anajua kuwa hatukuwa na maandalizi bora sana ya kabla ya msimu, lakini tulifanya kazi kubwa katika mchakato wa usajili na mmeona kuna baadhi ya wachezaji wakiwemo Djigui Diara, Aucho na Bangala ambao wameonesha uwezo mzuri, lakini naamini baada ya kuendelea kuwa pamoja watakuwa bora kuliko sasa.”


 Kwenye mechi hizo mbili Yanga imefunga mabao mawili na kuweza kukusanya pointi sita kibindoni na ipo nafasi ya pili kwenye msimamo kwa msimu wa 2021/22.

Namba moja ni Polisi Tanzania ambayo imeshinda mechi mbili na imefunga jumla ya mabao manne katika mechi hizo za mwanzo wa msimu wa ligi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic