LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea ikiwa ni mzunguko wa pili ndani ya msimu mpya wa 2021/22.
Viwanja viwili leo vitakuwa na kazi ya kuhimili vishindo vya Wanaume 22 ndani ya dakika 90.
Biashara United kutoka Mara watakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Ruvu Shooting, itakuwa Uwanja wa Karume, Mara.
Dodoma Jiji itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Simba kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Dodoma Jiji.
Dodoma Jiji ilishinda mchezo wake wa kwanza bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting huku Simba ikiwa imetoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Biashara United.
Mnyama lazima akalishwe leo mapema tu...
ReplyDeleteUlaaniwe wewe, uzao wako wote pamoja na kizazi chote cha Utopolo
DeleteHahahahaaaa tatizo la laana huzunguka na kurudi zilipotoka!! Ndio maana kulaani laani kumekatazwa
Delete