October 1, 2021

 


BAADA ya  Ligi Kuu Bara kuanza msimu wa 2021/22 kasi imekuwa kubwa kwa kila timu kupambana kusaka pointi tatu huku katika michezo iliyoshuhudiwa kwenye viwanja vitatu tofauti, ni Uwanja wa Karume ulikamilisha dakika 90 bila timu kupata bao.

Mchezo huo ulikuwa ni wa kukata na shoka kwa wawakilishi wa kimataifa kukutana uwanjani ambapo ilikuwa ni Biashara United wenyeji wanaopeperusha bendera kwenye Kombe la Shirikisho pamoja na Simba wanaopeperusha bendera kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na ulikamilika kwa ubao kusoma Biashara United 0-0 Simba.

Ni mabao 10 pekee yamekusanywa katika mzunguko wa kwanza ambapo kinara wa utupiaji kwa sasa ni Vitalis Mayanga na alifunga mabao yote mawili, Uwanja wa Karatu wakati timu yake ya Polisi Tanzania ikiwaadhibu KMC mabao 2-0 Uwanja wa Karatu.

Pia mchezo ambao ulishuhudia mabao mengi yakikusanywa ukiachana na ule kati ya Polisi Tanzania na KMC ni ule wa Namungo 2-0 Geita Gold Uwanja wa Ilulu Lindi ambapo nyota wa mchezo alikuwa ni Obrey Chirwa aliyetoa jumla ya pasi mbili za mabao.

Kwa upande wa waamuzi ni Rafaeil Ikambi aliyechezesha mchezo wa Polisi Tanzania na KMC alitoa jumla ya kadi tano za njano kwenye mchezo huo akimpoteza Emmanuel Mwandembwa ambaye alitoa kadi tatu kwenye mchezo wa Biashara United na Simba na pia huyu alishuhudia John Bocco akikosa penalti dakika za lala salama.


Imeandikwa na Dizo_Click

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic