MTENDAJI Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha Mazingisa, amesema kuwa jeuri ya wao kufanya vizuri msimu huu inatokana na kuwa na kikosi kipana ambacho anaamini kinatosha kuwapa mafanikio tofauti na msimu uliopita.
Akizungumza na Spoti Xtra, Senzo alisema: “Msimu uliopita tulikuwa tuna kikosi kimoja cha kukiamini pekee, yaani akiumia mchezaji tegemeo mmoja basi inakuwa tabu kubwa.
"Lakini msimu huu naamini kidogo tupo tofauti, hivyo tunatarajia kupata mafanikio kama kutwaa ubingwa wa ligi kuu.
"Najua haitakuwa kazi nyepesi bila kupambana, lakini tayari kama viongozi tumejitoa kuhakikisha mafanikio yanakuja ndani ya timu, hivyo tunahitaji kupewa ushirikiano mkubwa kutoka kwa mashabiki wetu na mambo mazuri yatakuja.”
Tayari Yanga imeanza msimu huu wa 2021/22 kwa ubingwa wa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Simba bao 1-0 Septemba 25.
Pia mchezo wao wa kwanza ndani ya msimu mpya wa 2021/22 ilishinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar na ina kazi kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Geita Gold, Uwanja wa Mkapa.
0 COMMENTS:
Post a Comment