WACHEZAJI wa Dodoma Jiji inayonolewa na Kocha Mkuu Mbwana Makata leo Oktoba Mosi wana kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.
Wakiwa kambini wachezaji hao wamekuwa ni wenye furaha kabla ya kucheza mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu Bara ambapo katika mchezo wa kwanza waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.
Wanakutana na Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ambaye ametoka kupata pointi moja mbele ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment