Ligi
Kuu ya Baraa inatarajiwa kuendelea wikiendi hii katika viwanja sita
tofauti nchini, viwanja vinne vikitimua vumbi kesho Jumamosi, na michezo miwili
kuchezwa siku ya jumapili.
Jumamosi
JKT Ruvu watakua wenyeji wa Coastal Union katika Uwanja wa Azam Complex uliopo
Chamazi jijini Dar es salaam, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakiwakaribisha
maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Timu
ya Mtibwa Sugar watawakaribisha Azam FC kwenye uwanja wa Manungu-Turiani mjini
Morogoro,nayo Ndanda FC watakua wenyeji wa timu ya Tanzania Prisons mjini
Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Ligi
hiyo itaendelea siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
Young Africans watawakaribisha timu ya Mbeya City kutoka mkoani Mbeya, huku
mjini Shinyanga katika uwanja wa Kambarage wenyeji timu ya Stand United
wakiwakaribisha maafande wa timu ya Polisi Morogoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment