Zlatan Ibrahimovic anaamini msema kweli ni kipenzi cha Mungu.
Ndiyo maana akaamua kuihama hotel ya Lowry ambayo hutumiwa zaidi na timu ya Manchester United na kuhamia Radisson Blu ambayo hutumiwa zaidi na kikosi cha Man City.
Uamuzi wake wa kuhama hotel aliyopangiwa wakati anatafutiwa nyumba ni kwamba haina bwawa la kuogelea.
BWAWA LA KUOGELEA LA HOTELI YA RADISSON |
Yeye alikuwa anaishi katika hoteli hiyo pamoja na familia yake. Huku wakiendelea kusubiri wapate nyumba wanayotaka na zoezi la madalali linaendelea.
Lakini akaona hakuna hata bwawa la kuogelea na familia yake inalihitaji. Hivyo hakuwa na zaidi ya kusema anahamia katika hoteli yenye bwawa la kuogelea bila ya kujali kwamba Man City huwa wakiishi hapo au vyovyote vile.
0 COMMENTS:
Post a Comment