February 18, 2013



 WAKATI WA ENZI, WAKIWA NA FURAHA...
Mwanariadha maarufu wa mbio za walemavu, Oscar Pistorius ambaye alishinda medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki iliyofanyika nchini Uingereza, imebainika alimpiga mpenzi wake risasi nne.
Pamoja na hivyo, tayari kuna taarifa zilizozagaa kwamba ugomvi wao ambao ulisababisha kifo cha Reeva Steenkamp ambaye ni mwanamitindo ilitokana na mwanadada huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mcheza raga maarufu, Francois Hougaard.
 PISTORIUS KAZINI....
Ingawa wakala wa Hougaard amekanusha lakini taarifa zinaeleza, Pistorius alishikwa na jazba baada ya kugundua mrembo huyo alikuwa na uhusiano na mchezaji huyo wa raga ambaye pia anakipiga katika timu ya taifa ya Afrika Kusini, Springbook.
Taarifa ya polisi wa mji wa Pretoria zimeeleza kuwa mwanariadha huyo alimpiga mrembo huyo risasi nne, moja kichwani, mkononi, kwenye hips na mguuni.
ANAYETUHUMIWA KUSABABISHA MFARAKANO HUO AKIWA KAZINI

Mwanadada huyo alijitahidi kukimbia baada ya kupigwa risasi ya kwenye hips na kujifungia chooni lakini mwanariadha huyo kutokana na hasira alipiga risasi mlango ukafunguka na kummalizia.
Tayari, Pistorius amepandishwa mahakamani na uchunguzi zaidi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo lililoshitua wengi katika nyanja ya michezo.
PISTORIUS MAHAKAMANI JUZI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic