Waafrika tunapenda soka, ndiyo mchezo tunaouamini na kuupenda
zaidi lakini umasikini wetu ni tatizo.
Kila mtu anayecheza mpira mtaani anatamani kuvaa jezi akapendeza
kama Ronaldo, Messi au wachezaji wa timu kubwa anawaona kwenye runinga.
Lakini uwezo wa kifedha ni tatizo, hii si Tanzania tu, kote barani
Afrika hasa nchi zilizo chini ya Jwangwa la Sahara.
Angalia picha hii ya kijana nchini DR Congo, inatia huzuni,
anatamani acheze soka akiwa amevaa protector au kilinda ugoko, lakini maisha ni
magumu, kaona aweke chupa.
Najiuliza, sijui chupa za glass au plastic? Kama ni glass maana
yake yuko hatarini zaidi kuliko kujilinda. Viatu alivyovaa, inaonyesha ndiyo vya mtoko na pia anachezea soka.
Ndiyo maisha yetu, lakini siku ya mwisho tunaishi na maisha
yanaendelea. Soka tunaendelea kuipenda na pamoja na umasikini wetu, tunaendelea
ku-enjoy.
MUNGU IBARIKI TANZANIA,
MUNGU IBARIKI AFRIKA
Saleh Ally
0 COMMENTS:
Post a Comment