Kesi inaendelea...Kajala na mumewe..
Msanii
wa filamu, Kajala leo alihukumiwa miaka saba jela, au kulipa Sh milioni 13,
hali iliyozua hofu na mshangao huku wengi wakiwa hawajui watamuokoa vipi.
Lakini
msanii mwingine maarufu wa filamu, Wema Abrahamu Sepetu alijitokeza na kumwaga
Sh milioni 13 na kumuokoa Kajala ambaye alipata pigo baada ya mumewe Faraji
Agustino kwenda gerezani.
Agustino
alihukumiwa kwenda jela miaka saba au fedha Sh milioni 200 ambazo zilikosa
mlipaji, hivyo akapanda karandika kwenda kuanza maisha ya gerezani.
Kajala
alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe huku Agustino akiwa na
msala wa kutakatisha fedha haramu.
Dakikia
chache baada ya huku ya Kajala, Wema ambaye alishauriana na wasanii wenzake
akiwemo baba mzazi wa Kajala, Mzee Masanja na mambo kuoneakan yamezidi unga.
Msanii
huyo maarufu, muda mwingine alionekana kutafakari wakati mjadala ukiendelea,
kabla ya kuondoka na kwenda benki ambako alichota mkwanja huo na kurudi na
kumkomboa Kajala.
Wasanii
mbalimbali walijitokeza leo katika mahakama ya Kisutu jijini Dar, akiwamo
Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye aliongozana na mama yake mzazi.
Pia
Dk Cheni ambaye alishiriki katika juhudi za kuhakikisha Lulu anapata dhamana
kutokana na kesi yake inayomkabili ya tuhuma za mauaji ya Steven Kanumba.
0 COMMENTS:
Post a Comment