Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika mechi za fainali ya mashindano ya 10 ya Kombe la Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Mratibu
wa mashindano hayo, Juma Kintu alisema jana kuwa, fainali hizo za soka na
netiboli, zitachezwa kesho kwenye uwanja wa klabu ya Sigara, Chang'ombe, Dar es
Salaam.
Kintu
alisema katika mechi hizo za fainali, Changamoto itamenyana na Jambo Leo wakati
katika netiboli, TBC itamenyana na BTL.
Changamoto
ilifuzu kucheza hatua hiyo juzi baada ya kuichapa IPP kwa penalti 4-3 wakati
Jambo Leo iliitoa TBC kwa kuichapa mabao 2-0.
Katika
netiboli, BTL ilifuzu kucheza fainali baada ya kuichapa Tumaini mabao 51-9
wakati TBC iliwalaza wenyeji NSSF kwa mabao 28-17.
Kintu
alisema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mechi hizo za fainali yamekamilika
na amewataka wafanyakazi wa vyombo vya habari vilivyoshiriki katika mashindano
hayo kujitokeza kwa wingi kwenye sherehe za ufungaji.
Bingwa wa
michuano hiyo kwa upande wa soka atazawadiwa kitita cha sh. milioni nne,
mshindi wa pili sh. milioni tatu wakati mshindi wa tatu atapata sh. milioni
1.5.
Kwa
upande wa netiboli, bingwa atazawadiwa sh. milioni tatu, mshindi wa pili
atapata sh.milioni mbili na wa tatu sh. milioni moja.
Wafungaji
bora wa michezo yote miwili watapata zawadi ya sh. 300,000 kila mmoja.
Mashindano
hayo yalifunguliwa rasmi Machi 9 mwaka huu na Waziri wa Kazi na Ajira,
Gaudencia Kabaka. Timu 17 kutoka vyombo mbalimbali vya habari zilishiriki
katika mashindano hayo.
Timu hizo ni Habari Zanzibar, Changamoto, Free
Media, TSN, Redio Kheri, IPP, BTL, Uhuru Media, Mlimani TV, Tumaini, Global,
Jambo Leo, TBC, New Habari, Mwananchi, Sahara na wenyeji NSSF.
0 COMMENTS:
Post a Comment