Mlezi
wa Simba, Rahma Al Kharusi leo mchana aliamua kurudisha nguvu zake kwa watoto
yatima baada ya kuwatembelea na kula na kunywa na watoto wa kituo cha Umra cha
Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam.
Akiwa
katika kituo hiyo, Rahma maarufu kama Malkia wa Nyuki, akiwa ameongozana na
mwanaye, Fatma walijumuika pamoja na kunywa na kula na watoto hao pamoja na
maofisa wa vituo hicho.
Pamoja
na kula na kunywa na watoto hao, Malkia wa nyuki alitoa misaada ya vyakula,
vinywaji, unga, mafuta kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya kila siku.
Pia
Malkia wa nyuki aliahidi kuwafanyia ukarabati nyumba yao iliyo katika eneo la Mbezi
Msakuzi, nje ya jiji la Dar es Salaam.
Wakati
akiwa kituoni hapo, watoto walionekana kuwa na furaha hasa baada ya kugawiwa
jezi nyekundu zenye namba tofauti mgongoni na jina la Malkia.
Watoto
hao walionyesha kufurahia ugeni huo kwa kucheza pamoja na mama huyo ikiwa ni
pamoja na kuimba nyimbo mbalimbali huku wakionyesa vidole vitano, ‘hata sijui
walikuwa wanamaanisha nini’.
Malkia
alisema hiyo imekuwa ni kawaida yake kuwatembelea watoto wenye matatizo mara
kadhaa kwa lengo la kuwafariji na kuwaonyesha kwamba pamoja na yote, lakini
wapo watu wanaowakumbuka.
Lakini
pia ni katika kufuata misingi ya dini, kuwasaidia wenye matatizo hata kama
utakuwa nacho kitu kidogo tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment