Bocco akichuana na Chuji..
Mshambuliaji
nyota wa Azam FC, John Bocco na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wamekwama
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa muda.
Wakati
Azam FC imetua nchini leo asubuhi ikitokea nchini Liberia ilipokwenda kuivaa
Barrack ya huko, Bocco na wengine kadhaa wamelazimika kusubiri uwanjani hapo.
Kwa
mujibu wa uongozi wa Azam FC, Bocco na wenzake watalazimika kusubiri ndege
itakayoondoka leo mchana huko kurejea nyumbani.
Azam
imelazimika kuwasili nchini kwa mafungu baada ya ratiba hiyo ya Shirika la
Ndege la Kenya maarufu kama KQ kuwa na mchanganyiko huo.
Azam
FC ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Caf, wamewasili
nchini na kupokelewa kama mashujaa baada ya kushinda kwa mabao 2-1 ugenini
mjini Monrovia.
Hata
hivyo, kazi haijaisha dhidi ya Waliberia hao kwani Azam FC italazimika kuulinda
ushindi wao katika mechi ya marudiano jijini Dar es Salaam au itakwama.
0 COMMENTS:
Post a Comment