Washambuliaji wawili wa TP Mazembe,
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wametua nchini na moja kwa moja wamejiunga
kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars.
Samatta na Ulimwengu wamewasili nchini
wakitokea Lubumshashi, DR Congo jana saa 3 usiku na ndege ya Shirika la Ndege
la Kenya maarufu kama KQ.
“Kweli wamejiunga na wenzao, tuko nao
kambini na kwangu ni kitu kizuri sana kwa kuwa nilikuwa ninawahitaji kwa wakati
huu,” alisema
Stars inatarajia kuivaa Morocco
wikiendi hii kuwania kucheza Kombe la Dunia, mechi inayotazamiwa kuwa kali na
ya kusisimua.
Tayari Stars ilishaanza kambi jijini
Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu kushinda ili kujiweka
katika nafasi nzuri ya kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.
Poulsen amekuwa akiwatumia
washambuliaji hao kwa mtindo tofauti, mara nyingi amekuwa akianza na Samatta na
Ulimwengu huingia kipindi cha pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment