Mwamuzi Msaidizi wa zamani wa kimataifa wa
Tanzania, Leslie Liunda ameteuliwa kuwa mtathimini wa waamuzi (referee
assessor) kwenye moja ya mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
limemteua Liunda kutathimini waamuzi kwenye mechi kati ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Libya itakayochezwa Jumapili (Machi 24 mwaka
huu).
Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Martyrs
jijini Kinshasa kuanzia saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika ya Kati (CAT).
Waamuzi watakaochezea mechi hiyo William Selorm
Agbovi atakayekuwa mwamuzi wa kati, Malik Alidu Salifu (mwamuzi msaidizi namba
moja), David Laryea (mwamuzi msaidizi namba mbili) na mwamuzi wa mezani (fourth
official) Cecil Amatey Fleischer. Waamuzi wote hao wanatoka Ghana.
0 COMMENTS:
Post a Comment