Wakazi wa maeneo ya Buseresere na Katoro wameomba michuano ya
Amani na Upendo iwe kila mwaka.
Ombi hilo lilitolewa na wanakijiji wa eneo hilo, muda mchache
baada ya kumalizika kwa fainali ya michuano hiyo iliyofanyika na kuishia kwa
Katoro kuibuka mabingwa kwa kuichapa Buseresere kwa mikwaju ya penalti 5-4.
Ombi hilo lilifikishwa kwa waandaaji ambao ni gazeti la
Championi na Mhariri wake Kiongozi, Saleh Ally alisema wanalifanyia kazi na
huenda kukawa na jibu zuri.
“Kumekuwa na mafanikio makubwa na tumeona wenzetu wa eneo
hili wameipokea michuano hii kwa mikono miwili. Ni gharama kubwa lakini
tutalifanyia kazi na imani kubwa itakuwa michuano endelevu,” alisema.
Wakati wa michuano hiyo, mashabiki walikuwa wakijitokeza kwa
wingi sana na kuzishangilia timu zao kwa nguvu zote.
Michuano hiyo imeandaliwa ili kurejesha upendo na amani
miongozi mwa wakazi wa eneo hilo baada ya vurugu za suala la uchinjaji
zilizozababisha mchungaji kuuwawa na muumini mmoja mwislamu kujeruhiwa kwa
risasi.
0 COMMENTS:
Post a Comment