Pamoja na kulazimika kitandani kwa siku mbili kutokana na
kusumbuliwa na homa pamoja na mafua makali, Malkia wa Nyuki amesema ataongozana
na kikosi cha Simba hadi Kagera na Mwanza.
Rahma Al Kharusi amesema ameamua kuungana na timu hiyo ili
kuongeza nguvu katika mechi mbili ambazo ni muhimu sana.
“Kweli ninaumwa, nimelazimika kukaa ndani tu hata shughuli zangu nimeshindwa kufanya. Lakini naona nitalazimika kwenda Bukoba kwa kuwa Simba inakwenda na kuna mechi
ngumu.
“Mechi hizo mbili ni muhimu sana kwetu, lazima tushinde. Lakini
haitakuwa lahisi, hivyo nitaungana na vijana na Wanasimba wote watakaokuwa huko
tukapambane.
“Lazima Kagera ni timu nzuri na itakuwa kwao, sisi tutakuwa
na timu ya vijana zaidi, lakini walicheza vizuri mechi na Coastal Union ambao
pia ni wazuri,” alisema Malkia wa Nyuki.
Baada ya kuivaa Kagera, siku mbili baadaye Simba itarejea jijini Mwanza na kuivaa Toto African iliyo katika wakati mgumu wa kuteremka daraja na lazima itapambana kuokoa 'roho' yake.
Malkia wa Nyuki ndiye amekuwa mhimili mkubwa wa Simba baada
ya baadhi ya viongozi wake kuonekana kupoteza dira.
Mwanamama huyo amekuwa tegemeo katika masuala ya ushauri pia
kifedha na wanachama na wadau wamekuwa wakitaka apewe sapoti kutokana na
anavyojitolea.
0 COMMENTS:
Post a Comment