Kipa wa Simba, Juma Kaseja ameonyesha ni mtu mwenye
ushirikiano na wachezaji wenzake baada ya kutoa mafunzo ya uhakika kwa makipa
makinda wa timu hiyo.
Kaseja ‘raia’ wa Kigoma alifanya hivyo wakati wa mazoezi ya
timu hiyo, lakini akaonekana ni kivutio zaidi kwa mashabiki waliojitokeza
mazoezini hapo kutokana na ufundishaji wake.
Mara kadhaa, Kaseja alikuwa akiwaelekeza wachezaji hao
makinda namna ya kuchutama kwa mipango na kuwa na tahadhari ya wapi mpira
utapigwa.
Alitaka wachuchumae, wakashindwa hivyo akalazimika kuwashika
makalio ili kuwatafutia balansi. Lakini hapo, maneno yakaanza.
Hata hivyo, Kaseja aliyeonekana kuelewa kinachoendelea,
alizidi kuwa siriaz na kuifanya kazi yake kwa ufanisi zaidi.
Kaseja anaamini ndiye kipa bora zaidi wa kipindi hiki na
baadhi ya wasaidizi au wanafunzi wake kama Ally Mustapha ‘Barthez’, Deogratius Munishi
‘Dida’ wamekuwa wakijitahidi kumpa upinzani.
0 COMMENTS:
Post a Comment