Kiungo
wa pembeni wa Yanga, Nizar Khalfan ameanza mazoezi ya taratibu ikiwa ni siku
chache tokea alipoumia.
Nizar
aliumia wakati Yanga ilipokuwa ikipambana na Ruvu Shooting katika mechi ya Ligi
Kuu Bara, mechi ambayo aliibuka shujaa kwa kufunga bao pekee lililoipa Yanga
pointi tatu muhimu.
Katika
mechi hiyo, Nizar aligongana na mchezaji mmoja wa Ruvu Shooting, hali
iliyolazimisha atolewe kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
Daktari
wa Yanga, Nassor Matuzya amethibitisha Nizar kuanza mazoezi peke yake na
keshokutwa Jumatatu anatarajia kuungana na wachezaji wengine wa Yanga.
Nizar
ni kati ya wachezaji wazoefu walio katika kikosi cha Yanga na kadri siku
zinavyosonga mbele, Kocha Ernie Brandts amekuwa akizidisha imani kwake na kumpa
nafasi tofauti na ilivyokuwa awali.
Mchezaji
mwingine ambaye alikuwa ameanza mazoezi baada ya kukaa siku kadhaa nje kutokana
na kuumia ni beki Stephano Mwasyika.
Matuzya
amesema Mwasyika alishaanza mazoezi na Jumatatu atajumuika na wenzake kuendelea
na mazoezi ya kujiimarisha zaidi ili kurejea kikosini.
0 COMMENTS:
Post a Comment