Upasuaji wa beki wa Yanga, Ladslaus Mbogo umekuwa gumzo. Beki
huyo wamepasuliwa uvimbe mkubwa uliokuwa kwenye shavu lake.
Upasuaji huo ulifanyika kwenye hospitali ya Mwananyamala
jijini Dar es Salaam, jana na kuongozwa na Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya.
Baadaye wachezaji na viongozi walikwenda kumjulia hali Mbogo
ambaye alionekana kuwa na hali nzuri na mwisho kuanza utani na wenzake. Beki
huyo kajiunga na Yanga msimu huu akitokea Toto African ya Mwanza.
Mchezaji huyo anajulikana kwa jina la Mnyama na hivi karibuni
aliingia katika rekodi ya kupiga daruga hadi kuchana kiatu cha mshambuliaji wa
Yanga, Jerry Tegete.
Salehjembe inakuletea picha kutoka ndani ya chumba cha
upasuaji, hadi dakika chache kabla ya shughuli hiyo kuanza. Mwenyezi Mungu amsaidie Mbogo apone haraka na kurejea uwanjani aendelee na majukumu yake.
Kabla upasuaji haujaanza...
Tayari kwa kuanza upasuaji...SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment