Pamoja na kutoswa na klabu ya Simba, mshambuliaji Danny
Mrwanda ameanza kuonyesha makali yake akiwa na timu yake mpya ya Da Nang FC ya
Vietnam.
Mrwanda ameanza vizuri na klabu yake hiyo mpya baada ya
kufunga bao moja kati ya matatu timu yake iliyopata wakati ikipambana na
Kantalan ya Malaysia katika michuano ya Asia Cup.
Da Nang FC ikiwa nyumbani ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa
mabao 3-2 huku Mrwanda aliyejiunga nayo msimu huu akifunga la kwanza.
Timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo, safari hii akina
Mrwanda watakuwa ugenini Malaysia.
Mrwanda alitoswa na Simba katika hatua za mwisho baada ya
kuonekana kiwango chake si kizuri.
Lakini yeye alisisitiza kuwa alikuwa ameongezeka uzito kwa
kuwa baada ya kumaliza mkataba wake na Long Dont Tam hakufanya mazoezi ya
kutosha, hata hivyo hawakumsikiliza na kuamua kuachana naye.
0 COMMENTS:
Post a Comment