Benchi la ufundi la timu ya taifa ya Morocco
limeamua kufanya mazoezi katika uwanja maalum ya ndani kwa ajili ya kukabili
Taifa Stars Jumapili hii.
Uamuzi huo unatokana na taarifa walizopenyezewa
kwamba mwechi dhidi ya Stars itachezwa mchana wa jua kali jijini Dar es Salaam.
Kutokana na hofu ya kuathiriwa na joto, kikosi
hicho kilifanya mazoezi kwenye uwanja wa ndani ambao unakuwa na hali ya joto.
Hali ya hewa na mji wa Rabat, Morocco imekuwa kati
ya nyuzijoto 12 na 13 kwa siku tatu mfululizo wakati Dar es Salaam inaanzia
nyuzijoto 26 hadi 30.
Pia wachezaji wengi wa kikosi hicho cha Morocco wanacheza soka la kulipwa katika nchi za Ulaya, hasa Ufaransa na Belgium.
Morroco imefania kushinda mechi hiyo dhidi ya Stars
ili kujiweka vizuri lakini kuna hali ya hofu hasa baada ya kikosi hicho cha Kim
Poulsen kuwaadhibu waliokuwa mabingwa wa Afrika, Zambia na vigogo, Cameroon.
0 COMMENTS:
Post a Comment