Enzi za Moro United ya Ligi Kuu Bara...
Timu ya Moro United iko katika kundi la tatu zilizoshuka
daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kurudi Ligi ya Mkoa msimu ujao wa
2013/2014 baada ya kushika nafasi za mwisho katika ligi hiyo msimu huu
2012/2013 iliyomalizika wikiendi iliyopita.
Moro United iliwahi kuwa moja ya timu vigogo Ligi Kuu Bara
wakati ikiwa chini ya mmiliki wake aitwaye Melley Balhabou.
Wachezaji kadhaa nyota walitokea katika timu hiyo akiwemo
kipa nyota zaidi nchini, Juma Kaseja ambaye sasa ni nahodha wa Simba, Gaudence Mwaikimba wa Azam FC,
Oscar Joshua na Nizar Khalfan wa Yanga. na wengine wengi wanaoendelea kufanya vizuri wakiwa na timu nyingine.
Moro United kutoka kundi B baada ya kumaliza mechi zake
ikiwa na pointi tatu. Wakati kutoka kundi C timu iliyoshuka ni Morani ya
Manyara iliyomaliza ligi ikiwa na pointi kumi na moja.
Small Kids ya Rukwa imeporomoka kutoka kundi A baada ya
kuondolewa kwenye michuano hiyo mapema kwa kushindwa kufika uwanjani kwenye
moja ya mechi zake. Kwa mujibu wa kanuni matokeo yote ya mechi ilizocheza
yalifutwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment