Mshambuliaji
wa Azam FC, John Bocco amefanikiwa kuripoti kwenye kambi ya timu ya soka ya taifa,
Taifa Stars jijini Dar es Salaam.
Bocco
amefanikiwa kuripoti katika kambi hiyo baada ya kukwama jijini Nairobi kwa saa
kadhaa wakati akirejea nchini kutoka nchini Liberia ambako Azam FC iliichapa Barrack ya huko kwa mabao 2-1 katika mechi ya Kombe la Shirikisho.
Pamoja
na Bocco, wachezaji wengine wawili wa Azam FC, Aishi Manula na Mwadini Ally nao
waliliripoti pamoja na mshambuliaji huyo. Kabla ya hapo, Mcha Hamis paia wa
Azam FC aliliripoti mapema kwa kuwa alipata ndege mapema.
Bocco
alichelewa kutokana na Shirika la Ndege la Kenya kuwapangia ndege ambayo
ilitakiwa kuingia jijini Dar es Salaam mchana, huku wenzao wengine wakitangulia
na ndege iliyotua Dar asubuhi.
Kocha
Mkuu wa Stars, Kim Poulsen alisema baada ya wachezaji hao kuripoti, kikosi
chake kilikuwa kimekamilika na kilichokuwa kinafuatia ni maandalizi ya kuwavaa
Wamorocco.
“Kila
kitu safi sasa, familia imekamilika na tunachoendelea nacho ni mazoezi ya
pamoja kufikia tunachotaka. Nawashukuru sana vijana wangu kwa kuwahi kambini
hata waliochelewa walikuwa na sababu za msingi,” alisema Poulsen raia wa
Denmark.
0 COMMENTS:
Post a Comment