Tegete akiwa na Nsajigwa...
Mshambuliaji
wa Yanga, Jerry Tegete ameondolewa kwenye ratiba ya mazoezi magumu ili apunguze
maumivu ya goti.
Wakati
wenzake wakiendelea na mazoezi ya kawaida, Tegete atalazimika kufanya mazoezi
ya kawaida na mepesi ili aweze kuendelea na matibabu ya goti.
Daktari
wa Yanga, Nassor Matuzya amesema hali hiyo inatokana na maumivu makali ya goti
ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa kipindi kirefu kidogo sasa.
“Atakuwa
anaendelea na matibabu lakini hatafanya mazoezi magumu kwa kipindi fulani. Baada
ya hapo tutakuwa tukiangalia anaendelea vipi ili kujua nini cha kufanya,”
alisema Matuzya.
Tegete
amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti ambayo amewai kueleza yanamyima raha
uwanjani na kusababisha acheze huku akiwa ana hofu.
Hivi
karibuni ameingia katika lawama kubwa pamoja na washambuliaji wengine ya kukosa
mabao mfululizo katika mechi zao wanazocheza.
Safu
ya ushambuliaji ya Yanga imekuwa ikikosa mabao mfululizo katika mechi zao za
Ligi Kuu Bara, hivyo kusababisha timu hiyo inayoongoza ligi kushinda mechi nne
mfululizo kwa idadi ya bao moja tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment