March 18, 2013




 
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Hamza Said (Zola).


Mamia ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa soka leo jioni wameshiriki katika safari ya mwisho ya kuusindikiza mwili wa aliyekuwa mfanyakazi wa klabu ya Yanga marehemu Hamza Said (Zola), mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.

Mazishi ya Zola yaliongozwa na makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga, muasisi wa klabu ya Yanga Mzee Jabir Katundu, aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga wakili Iman Madega na viongozi wengine mbalimbali waliowahi kuongoza klabu ya Yanga.

Marehemu Zola ambaye alifikwa na umauti jana alfajiri katika makutano ya mitaa ya Rufiji/Congo kwa ajali ya kugongwa na gari, alikua akitokea mitaa ya kariakoo akitembea kuelekea makao makuu ya klabu na ndipo gari hilo lilipomgonga kwa nyuma wakati akitembea kuelekea klabuni.

Mwili wa marehemu Hamza Said (Zola) ukiwasili makao makuu ya klabu kwa ajili ya kuangwa na wapenzi wa soka, washabiki na wanachama
Uongozi unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na wapenzi wa soka nchini kwa kuondokewa na rafiki yetu kipenzi.  

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic