March 18, 2013



Okwi akiwa mazoezini na Etoile du Sahel ya nchini Tunisia..
 
Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi tayari ameanza kukonga nyoyo za Waarabu wa Tunisia.

Okwi raia wa Uganda, amejiunga na Etoile du Sahel ya Tunisia akitokea Simba ‘bure’ kwa kuwa hadi sasa hakuna kilicholipwa pamoja na ahadi yad ola 300,000.

Akizungumza na mtandao huu, Katibu Mkuu wa Etoile du Sahel, Adel Githi amesema wana matumaini makubwa na Okwi.
Githi amesema Okwi ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa, kinachotakiwa ni kumpa muda badala ya haraka.


“Sisi tunafanya mambo mengi pia kwa kuangalia muda, Okwi ni mmoja wa wachezaji bora kabisa.
“Tunampa muda na atakuwa akiendelea na mazoezi hadi tutakapohakikisha yuko fiti kabisa. Kwa sasa yuko na wenzake na anafanya mazoezi vizuri tu.

“Tunaamini alikuwa ni chagua sahihi na tutaendelea kumuunga mkono ili kuendeleza kipaji chake kwa faida ya klabu na yake binafsi kama mchezaji,” alisema Githi.

Okwi amekuwa akiendelea kufanya mazoezi bila ya kucheza mechi, lakini kila siku zinavyosonge amekuwa akizidi kuonyesha makali yake taratibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic