Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho
Kikwete, jana alitembelea na kuuzindua Uwanja wa Chamazi Complex unaomilikiwa
na Azam FC.
Katika ziara hiyo, Kikwete maarufu kama JK alikabidhiwa jezi
ya Azam FC ambayo timu huitumia ugenini na mchezaji aliyepata bahati Rais
Kikwete kutumia jezi yake ni Ibrahim Mwaipopo.
Kikwete alikabidiwa jezi namba 4 ambayo hutumiwa na kiungo
huyo mkabaji wa Azam FC, haikujulikana mara moja kwa nini rais alipewa jezi
yenye namba hiyo.
Lakini pia haikujulikana kwa nini Rais Kikwete alikabidiwa
jezi ya ugenini inayotawaliwa na rangi ya njano badala ya ile ya nyumbani
inayotawaliwa na rangi nyeupe?
Akiwa eneo hilo, Kikwete alitembelea maeneo mbalimbali ya
uwanja huo na wakati wa hotuba yake aliwapongeza Azam FC kutokana na hatua
kubwa waliyopiga huku akiwataka Simba na Yanga au timu nyingine za wanachama
kuiga mfano.
Pia aliwataka kubadilika na kuacha maneno mengi au kutegemea
klabu ziwasaidie wao badala ya wao kuzisaidia.
0 COMMENTS:
Post a Comment