Peter Ndlovu..
Mshambuliaji
wa zamani wa Coventry, Birmingham na Sheffield United, Peter Ndlovu raia wa Zimbabwe
amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kusababisha kifo cha kaka yake.
Ndlovu
alikuwa anaendesha gari wakati ajali mbaya ilipotokea na kusababisa kifo cha
kaka yake, Adam Ndlovu pamoja na rafiki yake.
Gari baada ya ajali...
Katika ajali
hiyo ya gari aina ya BMW X5 lililogonga mti karibu na uwanja wa ndege ulio
karibu na maporomoko ya Victoria, Ndlovu aliumia vibaya kichwani na mguuni.
Wakati wa
mazishi ya kaka yake, Ndlovu mwenye miaka 39 alihudhuria akiwa katika kiti cha
matairi kutokana na kushindwa kutembea.
Marehemu Adam Ndlovu (kulia), enzi za uhai wake..
Ukiachana
na Adam ,42, aliyefariki katika ajali hiyo, mwingine aliyefariki alikuwa ni Nomqhele
Tshili aliyekuwa na miaka 24.
Wakati ajali
inatokea, Ndlovu alikuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Zimbabwe pia kocha
mkuu wa timu ya vijana chini ya miaka 23.
Marehemu Adam
alikuwa mmoja wa wachezaji nguli wa Zimbabwe aliyecheza soka la kulipwa katika
nchi za Switzerland na Afrika Kusini pia alishikilia rekodi ya ufungaji mabao
katika timu ya taifa ya Zimbabwe na baadaye alipostaafu akachukua jukumu la
kuifundisha timu ya ligi kuu nchini mwaka ya Chicken Inn.
0 COMMENTS:
Post a Comment