Wachezaji
wa Simba, jana walikiona cha moto katika mazoezi ya timu hiyo kwenye Viwanja
vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kocha
Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kikhwelo ‘Julio’ alisimamia zoezi la wachezaji hao wakati
wanakimbia kwa kasi kubwa kuuzunguka uwanja.
Upande
wa pili alikuwepo Kocha Mkuu, Patrick Liewig na muda mwingi Julio ndiye alikuwa
anafanya kazi ya kuhamasisha huku akiwataka wachezaji kuongeza kasi.
Mazoezi
hayo yalikuwa magumu na Julio alipoulizwa kisa cha yeye kufanya mazoezi hayo,
alisema wachezaji wengi wa Tanzania wana uwezo.
“Sasa
kama una uwezo halafu hauna pumzi unafikiri unaweza kucheza, haiwezekani.
Wachezaji wengi wa Tanzania wana uwezo. Pia mpira uucheze kwa raha, lazima uwe
fiti,” alisema Julio.
Mazoezi
hayo yaliendelea kwa saa kadhaa, kabla ya kutoa ruhusa ya kumaliza na baada ya
mazungumzo mafupi, wachezaji walipewa ruhusa kurejea makwao.
0 COMMENTS:
Post a Comment