Mkongwe katika soka ya Tanzania, John Tegete amesema Ligi Kuu
Bara inakosa ushindani kutoka katika timu za mikoani kutokana na ukata.
Tegete ambaye ni baba wa mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete
amesema ukata katika klabu mbalimbali za mikoani umekuwa ni tatizo kubwa.
“Timu za mikoani zina vipaji sana, lakini tatizo kubwa
limekuwa ni ukosefu wa fedha. Ukata unaziua timu za mikoani,” alisema.
“Hata makocha, wazuri ni wengi sana mikoani, lakini
wanaangukia katika hali mbaya ya kifedha. Mazingira ya kazi ni magumu sana
lakini watu wanajituma sana.
“Nakuhakikishia Simba au Yanga kama wakipewa nafasi ya kuishi
maisha ya Toto au timu nyingine za mikoani kwa siku mbili tu, wachezaji wote
watakimbia,” alisema.
Mara kadhaa, Tegete amekuwa akilalamika kuhusiana na ukata ingawa
timu yake imekuwa ikitoa upinzani mkali kwa timu kubwa kama Yanga, Simba,
Mtibwa Sugar na Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment