Brandts akifafanua jambo kwa Saleh Ally...
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema pamoja na kufurahia ushindi dhidi ya Ruvu Shooting lakini bado hajafurahishwa na ushindi wa bao moja pekee.
Brandts raia wa Uholanzi amesema amesikitishwa na namna kikosi chake kinavyoendelea kupoteza nafasi nyingi za kufunga karibu kila mechi wanayocheza.
Lakini anaamini kujilina kupindukia pia ni sababu ya kikosi chake kushindwa kuibuka na ushindi mkubwa.
“Nina kikosi kizuri, wafungaji wenye uwezo mkubwa lakini namna tunavyokwenda siridhiki,” alisema Brandts.
Yanga ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufikisha rekodi ya kushindwa kwa bao 1-0 katika mechi nne mfululizo.
Yanga inahitaji angalau kushinda mechi nne mfululizo ili kujihakikishia kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara ambao unashikilia na watani wao Simba.
Hivi karibuni, Brandtts alilalam,a na tatizo la kupoteza nafasi za kufunga lakini akalaumu timu nyingi wanazokutana nazo kuonyesha zimepania kuishinda Yanga kwa kulinda kupindukia.
0 COMMENTS:
Post a Comment