March 13, 2013



Sababu ya kusema hizi ni jezi ghali ni kutokana na namna zinavyotangaza makampuni yaliyotoa fedha nyingi zaidi ili kuonekana kwenye vifua vya wachezaji wa timu husika.
Timu za soka za Ulaya, zinategemea mapato yake katika malipo ya runinga, viingilio pamoja na wadhamini. Ukiwapata walio tayari kutoa mikataba minono, basi inakuwa ni kheri au neema kwa klabu. 

Endelea kusoma uone klabu zinavyongiza mamilioni ya fedha ambayo yanatoa msaada mkubwa katika endeshaji.
 No 1: Barcelona, £25m kwa mwaka na Qatar Foundation
Barcelona walikubali dili la miaka mitano la pauni milioni 125m na kampuni ya Qatar Foundation, mkataba ulianza Desemba  2010 na kufanya uwe ghali zaidi baada ua Barcelona kuwa imejitolea na kulipa pia kuitangaza Unicef kwa miaka mitano. Kinachoonekana ni klabu hiyo kuvunja utamaduni wake wa kutokuwa na watangazaji lakini hali ya kiuchumi ikawalazimi kuichukua Qatar Foundation ambao ni Ng’O inayojihusisha na masuala ya elimu.

 No 2: Bayern Munich, £23.6m kwa mwaka na Deutsche Telekom
Hiyo ndiyo kampuni kubwa zaidi ya simu barani Ulaya, inawalipa Bayern Munich pauni milioni 23.6 kila mwaka, mkataba huo wa jumla ya pauni milioni 71m, unafikia tamati Novemba, mwaka huu. Haijajulikana kama wataongeza.

 No 3: Manchester United, £20m kwa mwaka, dili la miaka mine na Aon
Manchester United inaonekana kuyavutia makampuni makubwa zaidi ya bima ya Kimarekani, kabla walikuwa na AIG lakini sasa ni Aon iliyoamua kutoa mkataba wa miaka minne wenye jumla ya pauni 80 lakini kwa mwaka ni pauni milioni 20.
Mkataba huo ulianza kufanya kazi rasimi katika msimu wa 2010/11 baada ya Aon kuwapiku wapinzani wao AIG waliokuwa wanatoa pauni 14m kwa mwaka.


No 4: Liverpool, £20m kwa mwaka na Standard Chartered Bank
Achana na kwamba mambo hayawaendei vizuri kwenye Premiership, Liverpool ni klabu kubwa na ina mkataba mnono na Standard Chartered Bank kwa miaka minne. Awali wadhamini hao walitaka kuwadhamini Manchester United ambao pia ni wapinzani wakubwa wa Liverpool, ikashindikana.


 Real Madrid, £16.8m kwa mwaka na Bwin
Real Madrid ilikubali mtandao huo wa bahati nasiku wa Bwin kuwa wadhamini wao hadi Septemba, mwaka huu, kwa thamani mkataba huo hauna tofauti na ule wa Liverpool kwa thamani.

 No 5: Tottenham, £12.5m kwa mwaka na Autonomy na Investec
Ni makampuni mawili yaliyokubali kufanya kazi pamoja na mwisho kujitangaza na  Tottenham. Spurs watakuwa wakipata hadi pauni 20m lakini malipo ya dili hilo kwa mwaka ni pauni 12.5m.
Autonomy ni kampuni ya ujenzi huku ikifuatiwa na Investec ambayo ni benki na itakuwa ikijitangaza na klabu hiyo katika mechi zilizo chini ya Uefa na mechi nyingine kama Kombe la FA na lile la Ligi maarufu kama Capital.

 No 6: Chelsea, £10m na Samsung
Chelsea na Samsung wamekubaliana mkataba wa miaka mitatu ambayo itaisha mwishoni mwa msimu huu. Kampuni hiyo ya Korea Kusini imekuwa ikivutiwa zaidi na Chelsea na inaamini kumwaga pauni milioni 10 kila mwaka ni sahihi kwa Chelsea.
 AC Milan, £10m- na Emirates
Emirates walitangazwa kuwa wadhamini wapya wa AC Milan, kampuni hiyo kubwa ya ndege kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) walikubali kutoa pauni milioni 50 ikiwa ni pauni milioni 10 kila mwaka katika mkataba wao wa miaka mitano.

 No 7: Manchester City, £7.5m na Ethihad Airways
Air Ethihad wamechukua nafasi ya Thomas Cook kwa mkataba wa miaka mine utakaogharimu £30m. Dili hilo ni pauni million £7.5m kwa mwaka.

 No 8: Juventus, £6.7m na Betclic
Juventus wamekubali mkataba wa miaka miwili tu utakaogharimu pauni 13.4 kwa mwaka huku wakikubaliana na kampuni hiyo ya kamari ya Ufaransa, kwamba wanaweza kuongeza mkataba zaidi kama timu hiyo itafanya vizuri zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic