Wakati
wachezaji wa Simba waliokuwa katika kikosi cha Taifa Stars wamekwama jijini
Mwanza wakiwa njiani kwenda mjini Bukoba, Mlezi wao, Malkia wa Nyuki hatakwenda
kabisa.
Rahma
Al Kharusi, maarufu kama Malkia wa Nyuki ameshindwa kwenda Bukoba kuungana na
wachezaji wa Simba kutokana na kukwama kupata tiketi ya ndege ya kurudi jijini
Dar.
Akizungumza
na Salehjembe alisema amefanikiwa kupata tiketi ya kwenda pekee, wakati tiketi
ya kurudi imekuwa tatizo.
“Nimefanya
kila juhudi lakini imeshindikana kupata tiketi ya kurudi, nahofia nisije
nikakwama Bukoba wakati nina mikutano muhimu Dar na Zanzibar.
“Hivyo
naweza nisiende Bukoba kwa asilimia tisini, ila naendelea kujaribu kupata
tiketi hiyo,” alisema Malkia.
Wakati
mwanamama huyo nguzo katika kusaka ushindi kwa Simba anakwama kwenda, wachezaji
Juma Kaseja, Nassor Said ‘Chollo’, Shomari Kapombe, Amri Kiemba na Mrisho
Ngassa wako jijini Mwanza baada ya ndege kushindwa kutua Bukoba jana.
Ndege
zimeshindwa kutua kwenye uwanja wa mji huo kutokana na mvua kubwa zilizokuwa
zinaendelea kunyesha.
Kesho
Jumatano, Simba ina kazi ngumu dhidi ya Kagera Sugar, mechi ya Ligi Kuu Bara
ambayo ni muhimu kwa timu zote.
0 COMMENTS:
Post a Comment