Talib akiwa na kikosi chake cha timu ya Oman..
Kocha wa zamani wa Simba, Talib
Hilal ameendelea kuwanoa makocha na waamuzi mbalimbali wa soka la ufukweni
nchini Uganda.
Hilal ambaye aliwahi kuichezea
Simba wakati akiwa mwanasoka, ametoa mafunzo ya mchezo huo kwa wiki moja
kuanzia Machi 11 hadi 16.
Kocha hiyo imewapatia makocha na
waamuzi hao Waganda cheti cha Advance beach soccer kwa kuwa ni ya pili, mwaka
2001 alitoa mafunzo ya kozi ya mchezo huo ngazi ya cheti.
Akizungumza kutoka Kampala, alisema
Waganda wamepiga hatua kubwa katika mchezo huo kwa sasa ukilinganisha na
Tanzania.
“Wenzetu wamepiga hatua kubwa kwani
kwa miaka mitatu sasa wanazo ligi 5 kama Super League, University League, Women
League, Youth League na league ya makampuni.
“Wenzetu hawana beach lakini
wanatumia mchanga wa Lake Victoria, vipi sisi Tanzania tunazo best beach mpaka
leo hatujaanza? Inasikitisha sana. Huu mchezo kwasasa unakuja juu sana
unategemea kuwepo kwenye Olympic ya Brazil,” alisema Talib.
Kwa sasa Talib ni kocha wa timu
ya taifa ya Oman ya soka la ufukweni na ni kati ya timu zinazofanya vizuri
katika mchezo huo duniani.
Tanzania imekuwa ikiendelea
kusuasua katika mchezo na inaelezwa kuna kampuni imekabidhiwa kazi hiyo na TFF
lakini imekuwa ikiendelea kusuasua.
0 COMMENTS:
Post a Comment