Beki
wa kati wa Yanga, Ladslaus Mbogo atalazimika kusubiri hadi keshokutwa ili
kutolewa nyuzi katika shavu lake baada ya kufanyiwa upasuaji.
Wiki
zilizopita, Mbogo maarufu kama Mnyama alifanyiwa upasuaji wa uvimbe katika
shavu lake na hali yake imekuwa ikiendelea vizuri.
Daktari
wa Yanga, Nassor Matuzya amesema tayari Mbogo ameishatolewa utambi ambao
hutumika wakati wa oparesheni.
“Baada
ya utambi, litafuatia suala la nyuzi. Jumatatu itafanyika kazi hiyo na baada ya muda mambo mengine
yatafuatia,” alisema Matuzya.
Tayari
Mbogo ameruhusiwa kutoka katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam
ambako alifanyiwa upasuaji huo.
Uongozi
wa Yanga uliamua kuchukua uamuzi wa kumfanya Mbogo upasuaji huo ili kumsaidia,
kitu ambacho mchezaji huyo alitoa shukurani zake kama sehemu ya kumuongezea
mapenzi zaidi na klabu hiyo.
Mbogo
alijiunga na Yanga msimu huu akitokea Toto African ya Mwanza ambako alikuwa
mmoja wa mabeki wa kati tegemeo.
Kwa
upande wa Yanga, inaonekana analazimika kufanya kazi ya ziada ili kupata namba
katika kikosi cha kwanza chenye mabeki wa kati bora kama Kelvin Yondani ‘Cotton’,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Mbuyu Twite.
0 COMMENTS:
Post a Comment