Mlezi wa Simba, Rahma Al Kharusi amesema hataondoka jijini
Dar es Salaam kwenda Bukoba kuungana na wachezaji wengine wa Simba walio mjini
humo kusubiri mechi dhidi ya Kagera Sugar hadi atakapoondoka na wachezaji walio
katika timu ya taifa, Taifa Stars.
Manahoda wote wa Simba, Juma Kaseja na msaidizi wake, Shomari
Kapombe wako katika kikosi cha Taifa Stars. Wengine ni Nassor Said ‘Chollo’,
Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa. Stars inajiandaa kuwavaa Morocco Jumapili.
Rahma maarufu kama Malkia wa nyuki amesema atawasubiri
wachezaji hao ili aondoke nao kwenda Bukoba kwa ajili ya ‘vita’ hiyo dhidi ya
Kagera Sugar.
“Vijana wengine wametangulia na kwenda kujiandaa na mchezo
huo, lakini hawa wanabaki kwa ajili ya majukumu ya kitaifa. Nitawasubiri ili
niondoke nao pamoja.
“Nafikiri nitakachofanya ni kuondoka nao pamoja kwa ndege
hadi Kagera, tukiwa huko tutaongeza nguvu na kupambana pamoja,” alisema.
Malkia wa nyuki ndiye amekuwa muhimili mkubwa wa Simba ambayo
imekuwa ikiyumba hasa kutokana na uongozi wake kutokuwa makini.
Simba inalazimika kuishinda Kagera Sugar nyumbani wiki ijayo
ili kujiwekea uai wa kuendelea kuwania nafasi ya pili kwa kuwa ubingwa
unaonekana kama vile tayari una mwenyewe, Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment