Timu ya taifa ya Morocco wamewasili jijini Dar es Salaam leo
saa 9 alasiri, tayari kuivaa Stars katika mechi kuwania kucheza Kombe la Dunia, Jumapili.
Morocco ambaye ni moja ya timu bora barani Afrika ina kibarua
didi ya wenyeji wake Taifa Stars ambao tayari wako kambini kujiandaa na mechi
hiyo.
Wachezaji ambayo iliwasili jijini Dar es Salaam na dege la
Emirates walionekana ni wale wenye maumbo makubwa na nyuso za kujiamini.
Hata hivyo, Waarabu hao wa Afrika Kaskazini wanaijua kazi ya
Taifa Stars ambayo imekuwa haitabiriki hasa katika meci ngumu.
Morocco imekuwa ni kati ya timu zinazoisumbua Stars hata
inapokuwa nyumbani, kwani iliwahi kushinda bao 1-0, pasi ya kichwa iliyotolewa
na Marouane Chamakh ambaye sasa hayupo katika kikosi hicho kutokana na kudorora
katika kikosi cha Arsenal.
Kikosi cha Morocco, leo saa 11 jioni kitafanya mazoezi kwenye
Viwanja vya Gymkhana jijini Dar na kesho watakuwa kwenye Uwanja wa Taifa kama
sheria za Fifa zinavyoagiza, kwamba wageni wanafanya mazoezi kwenye uwanja
husika wa mechi, siku moja kabla ya mchezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment