Kama inavutiwa na mshambuliaji, Edison Cavani wa
Napoli, Man City imeambiwa itoe kitita cha pauni milioni 60 ambayo imetajwa kuwa ni nyingi sana.
Kocha Mkuu wa Man City, Roberto Mancini ndiye
amekuwa akivutiwa na mshambuliaji huyo ingawa chaguo lake la kwanza limeelezwa
kuwa Radamel falcao wa Atletico Madrid ya Hispania.
Uongozi wa Napoli umeonyesha hauna kipingamizi
kabisa na Cavani kutua Man City kama mabingwa hao wa England watakuwa tayari kumwaga
fedha hizo walizowatajia.
Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amesema
mchezaji anaweza kuamua kuondoka au kubaki.
“Inaonekana ni bei kubwa, bado tunamhitaji hapa,
uamuzi wa kuondoka uko mikononi mwake. Lakini tunahitaji malipo ya kiwango
hicho,” alisema De Laurentiis.
Cavani amekuwa tegemeo la ushambuliaji kwa Napoli
lakini inawezekana akakubali kuondoka kwa mambo mawili, kwanza maslahi na pili
kubadili mazingira.
0 COMMENTS:
Post a Comment