Wadudu nyuki ni hatari sana, hivi karibuni nusura
wasababishe mechi ya Ligi Kuu Brazil iahirishwe.
Nyuki hao walivamia uwanja na kuzua tafrani kubwa
wakati mechi hiyo ya ligi wiki iliyopita ikiendelea kati ya Ponte Preta dhidi
ya Atletico Sorocaba.
Mechi hiyo iliyokuwa ikichezwa iliyochezwa kwenye
Uwanja wa Moisés Lucarelli nusura iahirishwe kwa kuwa nyuki walizidi kuongezeka
na kusababisha hofu kubwa kwa watazamanji na hata wachezaji.
Lakini baadaye, nyuki walianza kupungua kwa kiasi
kikubwa lakini kundi chache likabaki lililokwenda kuweka kambi kwenye goli moja
la uwanja huo.
Kipa akawa hawezi kukaa langoni, hivyo wakalazimika
kuitwa wataalamu wa kuuwa nyuki ambao walifika na kufanya kazi hiyo na baada ya
hapo mechi hiyo iliyosimama kwa zaidi ya dakika 30 ikaendelea.
0 COMMENTS:
Post a Comment