Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Mebub Manji, leo jioni ameongoza uzinduzi wa baraza la
wadhamini wa klabu hiyo.
Miongozi
mwa wajumbe wa baraza hilo ni pamoja na
Balozi Ami Mpungwe, George Mkuchika pamoja na Francis Kifukwe aliyewahi kuwa
mwenyekiti wa Yanga.
Uzinduzi
huo ulifanyika kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga, mitaa ya Twiga na Jangwani
na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wengine wa Yanga kama Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na Katibu, Lawrance Mwalusako na waandishi wa habari.
Yanga
imeonekana kupiga hatua zaidi katika kudumisha umoja ndani ya klabu hiyo,
kuanzia uwanjani hadi katika masuala ya uongozi.
Mmoja
wa wajumbe wa baraza hilo ambaye hakuhudhuria ni Mama Karume ambaye imeelezwa
alikuwa safari nje ya nchi.
0 COMMENTS:
Post a Comment