Msuva, kushoto akiwa katika mazoezi ya Yanga kujiandaa na mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara
Mashabiki wa Yanga walionyesha kituko pale walipomvamia mshambuliaji
wao, Simon Msuva na kuanza kumtishia kuhusiana na ujio wa Mrisho Ngassa aliye
Simba.
Mashabiki hao walikuwa wakimueleza Msuva kwamba Ngassa
atakapowasili Yanga, basi namba kwake itakuwa ni tatizo na anapoendelea kukosa
mabao ndiyo atajiondoa.
Msuva alionyesha ustaarabu wa hali ya juu, pamoja na kushambuliwa
kwa maneno yakiwemo mengine yanayoudhi, lakini aliendelea kuwajibu vziuri na
mwisho akaingia katika basi la timu hiyo.
Kisa cha kumvamia ilikuwa ni kiungo huyo kukosa bao la wazi katika
mechi kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting.
Pamoja na timu yao kushinda mfululizo na kujichimbia kileleni,
mashabiki wa Yanga wamekuwa wakikerwa na kitendo cha ushindi wa bao 1-0 kila
mechi.
Yanga imeshinda mechi nne mfululizo kwa idadi hiyo ya bao 1-0,
kitu ambacho mashabiki hao wamekuwa wakilalama kupita kiasi.
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts naye amekuwa akionyesha kukerwa
na hali hiyo na hali hiyo ya ushindi finyu unaopatikana.
Ameahidi kwamba atalifanyia kazi suala hilo lakini bado limeng’ang’ania
ingawa bado Yanga inazidi kupaa kileleni kwa kuwa inazidi kuchukua pointi tatu
katika kila mechi.
0 COMMENTS:
Post a Comment