Mshambuliaji nyota wa Simba,
Felix Sunzu ameendelea kuwa katika sakata dhidi ya kocha wake Mfaransa, Patrick
Lieiwig.
Siku chache zilizopita, Liewig
alimfukuza Sunzu mazoezini kutokana na mchezaji huyo kutoweka bila ya taarifa
kwa zaidi ya siku nne, halafu aliporejea akataka kuanza mazoezini.
Liewig amesema Sunzu aendelee
kupumzika hadi hapo atakapomuita, hali ambayo imemlazimu mshambuliaji huyo raia
wa Zambia kuanza mazoezi kivyake.
Sunzu amesema amekuwa akiendelea
na mazoezi gym ili kuendelea kujiweka fiti na iwapo ataitwa mazoezini basi
ataungana na wenzake mara moja.
Taarifa zilieleza kuwa sunzu
aliondoka kwenda kwao Zambia kimyakimya, lakini yeye amekuwa akisisitiza
hakwenda na badala yake alijifungia kwake na kuzima simu.
0 COMMENTS:
Post a Comment