Takribani miaka 10 tokea winga
machachari wa zamani wa Yanga
afanye maajabu yake mjini
Kampala, Uganda lakini anaendelea kukumbukwa na wadau wengi wa soka.
Mchezaji wa zamani wa kimataifa
wa Uganda, Moses Basena amesema Lunyamila anakumbwa Uganda hadi leo.
“Labda kwa watu wa kizazi cha
sasa, lakini watu wa umri wangu au chini kidogo, wamekuwa wakiendelea
kumkumbuka Lunyamila.
“Nakumbuka kuna wakati hadi
magari mfano taxi (daladala) walikuwa wameandika jina lake nyuma. Yote hiyo
ilikuwa ni kuonyesha kukubali uwezo wake.
“Lunyamila alikuwa na uwezo
mkubwa sana, bado sijaona winga mwenye uwezo wake hapa Tanzania kwa kipindi
hiki,” alisema Basena.
Lunyamila aliiongoza Yanga mara
mbili mjini Kampala kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya vigogo
SC Villa waliokuwa wanaongozwa na nahodha, Paul Asule.
Lunyamila alikuwa akikabana na
Asule aliyekuwa beki wa kulia, shughuli aliyompa ndiyo imesababisha gumzo la
winga huyo lisiwe na mwisho.
Lunyamila ambaye ni mchambuzi
katika gazeti la Championi ni mmoja wa mawinga bora kabisa waliowahi kutokea
katika soka la Afrika Mashariki na Kati.
Lunyamila alikuwa na kasi kubwa
wakati akiwa Yanga, lakini baadaye alijiunga na Simba kabla ya kumalizia soka
lake Mtibwa Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment