Liewig akiondoka baada ya kuhakikisha Ismail akipanda bajaj...
Kinda Rashid Ismail ameendeleza
vituko, safari hii katika mazoezi ya Simba baada ya kuachana na kupanda basi la
klabu hiyo aina ya Yutong na badala yake akapanda zake Bajaj.
Ismail ambaye ni mtaratibu, mara
tu baada ya mazoezi ya Simba yaliyokuwa yamemalizika katika Viwanja vya
Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Aliamua kuacha basi liondoke.
Wakati Kocha Mkuu, Patrick Liewig
akiwa anasubiri usafiri alitaka kujua Ismail ataonoka vipi uwajani hapo.
Mara Bajaj yenye rangi nyekundu
iliingia kwa mbwembwe eneo hilo, ikapiga ‘turn’ na kupaki karibu kabisa na
Ismail.
Kuona hivyo, Liewig akamuuliza
Ismail kama huo ndiyo usafiri aliokuwa anasubiri, alipokubali, kocha huyo
alicheka na kutikisa kichwa kisha akaondoka na kusema: “umenichosha kabisa.”
Wakati huo, wachezaji wengine
walikuwa wameondoka na magari yao na baadhi wakipanda basi hilo lenye chata za
Kilimanjaro lililokuwa linapita mjini na baadaye Kariakoo.
Hivi karibuni, Ismail alihudhuria
kuangalia mazoezi ya Yanga mara mbili katika Uwanja wa Bora Kijitonyama na
kuzua gumzo.
Hata hivyo kinda huyo amekuwa
akisisitiza alikwenda kuangalia mazoezi katika uwanja huo wa Kijitonyama ambao
alichipukia kisoka.
0 COMMENTS:
Post a Comment