Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, leo amerejea nchini
akitokea India na kukumbana na tafrani kubwa kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Wakati Rage anawasili kutoka India alikokuwa amekwenda kupata
matibabu, baadhi ya mashabiki na wanachama wa Simba walifika uwanjani hapo
wakiwa kwenye basi aina ya Toyota Coaster wakiwa na mabango yanayomzodoa.
Mabango ya wanachama na mashabiki hao, yalikuwa yanamtaka
Rage aachie ngazi wakionyesa kuchoshwa naye.
Lakini waliimba nyimbo za
kumkejeli ambazo nyingine haziandikiki.
Lakini wakati wakiendelea na vurugu hizo, kuna mashabiki na
wanachama walikuwa wamefika uwanjani hapo kabla kumpokea Rage.
Ndipo tafrani kubwa likaibuka baina yao huku kila upande
ukitetea unachokiamini, lakini baadaye kundi lililokuwa pale kumpokea Rage
lilionekana kuwa na nguvu zaidi.
Waliokuwa wanataka Rage aondoke wakazidi nguvu na mapango ya
kumkashifu na kumtaka mwenyekiti huyo aondoke Simba yakachanwachanwa.
Baada ya Rage kutokea uwanjani hapo, mashabiki waliokwenda
kumpokea walimshangilia kwa nguvu lakini wale wasiomtaka walimzomea.
Joseph Itang’are maarufu kama Mzee Kinesi ndiye aliongoza
wanachama wa Simba kwenda kumpokea Rage.
Mwenyekiti huyo wa Simba aliye katika wakati mgumu na
shinikizo la kutakiwa kujiuzulu alikataa kuzungumza na waandishi wa habari na
kusisitiza atafanya hivyo Jumatano.
Tayari aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange ‘Kaburu’
ameishajiuzulu, hali inayozidi kumuongezea Rage shinikizo kubwa la kulazimishwa
kujiuzulu lakini yeye ameendelea kushikilia msimamo wake wa kuwa mwenyekiti.
0 COMMENTS:
Post a Comment