Wakati ina kibarua kigumu ugenini
dhidi ya Kagera Sugar, Simba imeamua kuchukua vijana wengi na kwenda kupambana
mjini Bukoba.
Simba inaondoka leo Jumamosi na
kundi la vijana hao kwenda kuwavaa Kagera Sugar ambao ni wagumu kama ‘nyundo’
wanapokuwa kwao.
Kocha Patrick Liewig amesisitiza
anawaamini vijana wake na ana imani watafanya vizuri.
“Nawaamini sana, matokeo ni kitu
kinachofuatia. Simba ina mpango wa muda mrefu na sasa kila anayepata nafasi
lazima acheze kwa ajili ya timu,” alisema.
Baadhi ya wakongwe walio katika kikosi hicho ni pamoja na Juma Kaseja, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba, Said Nassor 'Chollo', pia Kiggi Makasi.
Simba imeondoka bila
ya wakongwe kama Felix Sunzu, Abdallah Juma ambao wako kwenye mgogoro na kocha
Liewig.
Lakini imewaacha Paul Ngalema na
Amir Maftah wanaoelezwa kuwa ni wagonjwa lakini inaelezwa kuna mgogoro kati yao
na benchi la ufundi kama ilivyo kwa Mwinyi Kazimoto, Ramadhani Chombo, Haruna
Moshi ‘Boban’ na Juma Said Nyosso.
0 COMMENTS:
Post a Comment